TLP kuendelea kumuunga mkono JPM

0
302

Mwenyekiti wa Chama cha TLP Taifa, Augustino Mrema amesema kuwa chama hicho kitaendelea kumuunga mkono Rais John Magufuli, kwa kuwa kimeridhishwa na utendaji kazi wake hasa katika kuwaletea Watanzania maendeleo.

Mrema amesema hayo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mkutano mkuu wa TLP utakaofanyika Mei tano mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Mrema amepongeza uamuzi ya Rais Magufuli wa kukutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu jijini Dar es salaam, hatua ambayo amesema inakuza demokrasia ya kweli na kuongeza ushirikiano wa vyama vya siasa nchini.