The Royal Tour yamleta mwekezaji mkubwa wa Marekani

0
169

Jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kutangaza Utalii nchini kupitia Filamu ya Tanzania: The Royal Tour zinaendelea kuzaa matunda nchini.

Licha ya kupokea watalii wengi, Mwekezaji Mkubwa wa hoteli za Kifahari nchini Marekani Munir Walji amewasili nchini kwa lengo pa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana kuhusu uwekezaji wa Hotel za Kitalii ambazo zitaongeza thamani katika sekta ya hiyo ili kwenda na kasi ya ujio wa watalii wengi.

Katika mazungumzo yao Dkt. Chana amemshukuru na kumpongeza Walji kwa uwamuzi wa kutaka kuwekeza katika sekta ya Utalii hapa nchini na kumuahidi kumpa ushirikiano mkubwa ili aweze kufanikisha adhima yake njema kwa Tanzania.

Naye Walji ameipongeza Tanzania kwa kuweka Mazingira mazuri yanayo hamasisha na kuvutia wawekezaji katika sekta ya Utalii pamoja na kuvitangaza vyema vivutio vya Utalii hali inayoongeza idadi ya watalii.

Aidha, mwekezaji huyo amesema kuwa ameona ipo haja ya kuchangamkia fursa kwa kuwekeza kwenye sekta ya Utalii hapa nchini.