TFF yawafungia maisha kwa kupanga matokeo

0
500

Mwenyekiti wa Kitayose FC, Yusuph Kitumbo na Kocha wa mpira wa miguu, Ulimboka Mwakingwe wamefungiwa maisha kujihusisha na mpira wa miguu.

Adhabu hiyo iliyotolewa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa wanafamilia hao wawili wametiwa hatiani kwa kosa la upangaji matokeo.

Kitumbo na Mwakingwe walijihusisha na upangaji matokeo katika mechi za Ligi ya Championship kati ya Fountain Gate FC na Kitayosce FC iliyochezwa Aprili 29 mwaka huu mjini Gairo, Morogoro.