TFDA kuendelea kudhibiti usalama wa chakula

0
502

Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) imeweka mfumo maalum wa udhibiti wa usalama wa chakula kinachozalishwa ndani ya nchi  na kile kinachoingizwa kutoka nje,  ili kumhakikishia afya bora mlaji.

Akifungua semina ya siku mbili kwa waandishi wa Habari wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, – Adam Fimbo amesema kuwa mfumo huo unahusisha kufanya tathmini ya vyakula vilivyofungashwa,  kusajili maeneo na kutoa vibali vya biashara za vyakula.

Fimbo ameongeza kuwa,  mfumo huo pia unalenga kuchunguza sampuli za vyakula katika maabara.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani – WHO,  takribani watu Milioni 600 duniani huugua kila mwaka kutokana na kula chakula kisicho salama na kati yao Laki Nne na Ishirini Elfu  hufariki dunia.