Tetemeko laua watu 46

0
105

Idadi ya watu waliofariki dunia baada ya tetemeko la ardhi kukikumba kisiwa cha Java nchini Indonesia imefikia 46, na mamia wengine wamejeruhiwa.

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 5.6 katika kipimo cha matetemeko -Richter imelipiga hasa eneo la Cianjur lililopo magharibi mwa kisiwa hicho cha Java.

Tetemeko hilo la ardhi pia limeyatikisa maeneo kadhaa ya mji mkuu wa Indonesia, Jakarta na hivyo kulazimu baadhi ya watu wanaoishi katika majengo ya ghorofa kuhamishwa.

Maafisa wa uokoaji nchini Indonesia wamesema idadi ya watu waliofariki dunia inaweza kuongezeka, kwa kuwa watu wengi bado wamenasa kwenye
majengo pamoja na vifusi.