TET yatoa mafunzo kuhusu mtaala ulioboreshwa

0
139

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inaendelea kutoa mafunzo kwa walimu wakuu wa shule za msingi za Serikali na zisizo za Serikali, kwa lengo la kuwajengea uelewa wa namna bora ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali na Msingi wa mwaka 2023 ulioboreshwa.

Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema mafunzo hayo yanafanyika kwa walimu wakuu wote katika halmashauri 184 nchini kuanzia Mei 5, 2024 hadi Juni 12, 2024 kwa awamu tofauti ambapo katika awamu ya kwanza yatafanyika katika halmshauri za mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kagera Kigoma, Geita na Tabora.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa kuwa walimu wakuu wataweza kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake na kuweza kutoa msaada kwa walimu wengine pale inapohitajika.