Teknolojia kutumika kuinua mazao ya Mifugo

0
168

Serikali imewahakikishia wawekezaji wa vyakula vya mifugo Mazingira rafiki ya kuzalisha chakula chenye protini kwatumia teknolojia ya Kisasa ili kukidhi mahitaji ya wananchi wanaotegemea Mifugo kuinua kipato chao.

Hayo yameelezwa Wilayani Kigamboni na waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki wakati wa mkutano uliowakutanisha wazalishaji wa vyakula vya mifugo na wadau wa Mifugo kujadili namna ya kutumia Teknolojia mpya ya kuongeza Protini kwenye chakula cha Mifugo ili kutatua changamoto inayowakabili wafugaji wa Kuku na samaki.

Naye mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa amesema Teknolojia itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Wilaya hiyo na taifa kwa ujumla hasa ukizingatia kwamba wao pia wanafanya shuguli za Uvuvi na ufugaji kwa ajili ya kuongeza kipato chao cha kila siku.

Mkutano huo ambao umeratibiwa na ubalozi wa uholanzi nchini umehudhuri na wazalishaji pamoja na wasanbazaji wa chakula cha Mifugo kutoka Kenya na Tanzania.