TEA kuboresha miundombinu katika shule 151

0
193

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa imeainisha zaidi ya shilingi bilioni 8.6 kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 kwa ajili ya kugharamia ufadhili wa miradi 160 ya kuboresha miundombinu ya elimu katika shule 151 nchini.

Mkurugenzi mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amesema miradi hiyo inahusisha ujenzi wa madarasa 210 katika shule 70, maambara mbili za sayansi katika shule za sekondari zenye mahitaji maalum, matundu ya vyoo 2,040 katika shule 80, vifaa vya kujifunzia, kufundishia na uendelezaji wa miundombinu katika shule za watoto wenye mahitaji maalum.

Amewaambia Waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa, mbali na miradi ya Mfuko wa Elimu wa Taifa, taasisi hiyo inatekeleza mradi wa miaka mitano kuanzia mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021 unaotoa ruzuku za utekelezaji wa miradi ya kuendeleza ujuzi kutoka kwenye Mfuko wa Kuendeleza ujuzi.