TCU yavitaka vyuo vikuu kutumia mfumo wa TEHAMA kurahisisha ufundishaji

0
402

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa wito kwa vyuo vikuu vyote nchini kuhakikisha vinazingatia miongozo mbalimbali ya ubora ili kutoa wahitimu mahiri wanaokidhi vigezo vya ubora na mahitaji ya maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Katibu Mtendaji TCU, Prof. Charles Kihampa ameeleza kuwa ili kuhakikisha ufundishaji wa mitaala unakamilika ndani ya muda uliobaki katika mwaka wa masomo 2019/2020, vyuo vinashauriwa kutumia mbinu mbalimbali za ufundishaji ikiwemo matumizi ya TEHAMA bila kuathiri ubora.

Kufuatia maelekezo ya serikali ya kuvitaka vyuo vikuu vyote vifunguliwe Juni 1 mwaka huu, TCU imetoa muongozo na ushauri kwa vyuo hivyo kupitia mkutano wa dharura uliopitishwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mei 23, 2020 jijini Dodoma.

Aidha, Prof. Kihampa amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha jamii inahusishwa juu ya jambo hilo ili liweze kufahamika.