Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la udahili wa Shahada ya Kwanza kuanzia Agosti 26 badala ya Agosti 31 iliyokuwa imepangwa hapo awali.
Kufunguliwa huko kwa udahili kumekuja ikiwa ni siku 6 tangu Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2020, ambapo zaidi ya wanafunzi 70,000 walifaulu.
Kwa mujibu wa taarifa ta TCU, dirisha hilo litafungwa Septemba 25 mwaka huu na litahusisha makundi makubwa matatu ambayo ni mwenye sifa stahiki za kidato, wenye sifa stahiki za stashahada (ordinary diploma) au sifa linganifu na wenye sifa stahiki za ‘Foundation Programme’ ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
TCU imewataka waombaji wote kuepuka matapeli kwa kupata taarifa sahihi kutoka kwenye tovuti ya taasisi hiyo, kupiga simu au kutembelea ofisi zao.