TCU yafungua Dirisha la Udahili

0
330

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2019/20

Kwa mujibu wa taarifa ilitolewa katika tovuti ya tume hiyo udahili huo utafanyika kuanzia july 15 hadi Agosti 10, 2019.

TCU imetangaza kuanza udahili huo ikiwa ni siku chache zimepita tangu Matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2019 yalipotangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).