TBC yataka ushirikiano na vyombo vya habari DRC

0
155

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema kuna umuhimu wa kuanzishwa kwa ushirikiano baina ya waandishi wa habari wa TBC na wale wa Televisheni na Redio ya Taifa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Amesema ushirikiano huo utawawezesha wananchi wa pande zote mbili kupata habari za upande mwingine na pia utaimarisha ushirikiano wa muda mrefu wa mataifa hayo.

Dkt. Rioba ametoa kauli hiyo jijini Lubumbashi wakati wa kongamano la fursa za kibiashara na uwekezaji katika sekta ya TEHAMA kati ya Tanzania na DRC.

Ujumbe wa Tanzania katika kongamano hilo la siku mbili unaongozwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.