Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), leo limetembelea hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo jijini Dar es salaam kwa lengo la kutoa pole kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo pamoja na kutoa zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuonyesha upendo katika Siku ya Wapendanao ( Valentine’s Day).
https://www.youtube.com/watch?v=b_seGX5EJg0
Baadhi ya wagonjwa waliokutwa hospitalini hapo wameipongeza TBC kwa kuonesha upendo kwao na kuomba shirika hilo liendelee na moyo huo, huku wakiwapongeza madaktari na wauguzi kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wagonjwa.
Miongoni mwa zawadi zilizotolewa na TBC kwa wagonjwa hao katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni sabuni za kufulia na kuogea, mafuta ya kujipaka na dawa za meno.