TBC yapongezwa kwa utunzaji wa historia

0
175


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Rajabu Mabele ameeleza kufurahishwa na utunzaji wa kumbukumbu za Redio Tanzania Dar es salaam (RTD), ambayo kwa sasa ni TBC Taifa.


Brigedia Jenerali Mabele ametoa pongezi hizo mkoani Dar es salaam, alipotembelea banda la Shirika la Utangazaji (TBC), kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) baada ya kuona vifaa vya zamani vilivyokuwa vikitumiwa na RTD pamoja na nyimbo za zamani za wasanii wa Tanzania.

Pia ameishukuru TBC kwa ushirikiano wake na Jeshi la Kujenga Taifa, katika kuelimisha na kutangaza habari za Jeshi hilo.