TBC yapewa Tuzo

0
200

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limepewa Tuzo ya Utambuzi kwa kuwa mmoja wa wadhamini wa maonesho ya Swahili International Tourism Expo
(S!TE 2022).

Tuzo hiyo imetolewa leo katika maonesho ya Swahili International Tourism Expo yanayoendelea katika viwanja vya Mlimani City mkoani Dar es Salaam, ambayo yamefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.