TBC yapata tuzo kwa kutoa elimu ya watu wazima

0
206

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limepokea tuzo ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa wa utoaji elimu ya watu wazima kupitia vipindi mbalimbali kwa Watanzania

Tuzo hiyo imetolewa katika Kongamano la Kimataifa la miaka 50 ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania lililofanyika katika maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aidha, tuzo hiyo imetolewa kwa TBC baada ya kuwa mstari wa mbele katika kuelemisha watanzania kupitia redio na televisheni ambapo kupitia redio kulikuwa kukiandaliwa vipindi vya elimu ya watu wazima.

Katika hatua nyingine waandaaji wa kongamano hilo wametoa tuzo ya mchango wao katika kutoa elimu kwa jamii kwa viongozi na watu mashuhuri akiwepo aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere

Kongamano hilo la siku tatu limefunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambapo kaulimbiu yake ni Elimu ya Watu Wazima kwa Maendeleo Endelevu.