TBC yaadhimisha miaka 63 ya Rais Dkt. Samia

0
237

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha akipanda mti katika eneo la Vikonje mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

TBC kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeendesha kampeni ya kupanda miti nchi nzima, ili kuunga mkono jitihada na maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utunzaji wa mazingira.

Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja, Rajab Mkasaba ameshiriki zoezi la kupanda miti lililoratibiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 63 ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

TBC imeendesha zoezi la kupanda miti nchi nzima ikiwa ni kuunga mkono jitihada na maono ya Rais katika kutunza mazingira.