Baadhi ya Viongozi wa Shirika la Kimataifa la uhifadhi la Frankfurt Zoological Society wametembelea Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na kufanya mazungumzo na uongozi wa shirika hilo.
Frankfurt Zoological Society ni shirika linalojishughulisha na utunzaji wa bioanuai na kuhifadhi Wanyama pori pamoja na mazingira katika maeneo yaliyohifadhiwa.
Viongozi hao wa Frankfurt wamejadiliana na uongozi wa TBC masuala ya Wanyama pori na uhifadhi na namna ya kushirikiana ili kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii bila kusahau kundi maalum la watoto.
Aidha, uongozi huo wa Frankfurt umeipongeza Tanzania kwa kuwa kati ya nchi zinazohifadhi vizuri mazingira pamoja na wanyama pori.