Serikali imesema inasimamia kuhakikisha ujenzi wa mnara kwa ajili ya kurusha matangazo ya Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) unakamilika ifikapo Juni 2024 ili Wananchi wa wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa wafikiwe na matangazo hayo.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga aliyeuliza kwa kuwa upatikanaji wa mawasiliano unaenda sawa na uwekaji wa mkongo wa Taifa kufika, na kwa kuwa mchakato wa ujenzi wa mnara wa TBC umeshaanza, ni lini utakamilika ili Wananchi wa Kilolo wapete matangazo ya TBC kwa uhakika?.
Mhandisi Kundo ameongeza kuwa ni dhamira ya Serikali kuhakikisha wilaya zote nchini ifikapo Desemba 2014 zitakuwa zimefikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kwamba ifikapo Juni 2024 kata 99 zitakuwa zimefikiwa na mkongo huo.