TBC kuendana na kasi ya Teknolojia

0
176

Wizara ya habari teknolojia ya habari na mawasiliano imesema Dunia ya sasa inategemea sana TEHAMA katika kuendesha uchumi na maendeleo kwa ujumla na kuwa mapinduzi ya nne ya viwanda ni Teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA)

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano wa baraza la wafanyakazi wa TBC wa mwaka 2022 mkurugenzi wa TEHEMA katika Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Mulembwa Munaku amesema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) liendane na mabadiliko hayo

“Rais Samia Suluhu Hassan ameunda Wizara hii mahususi kwaajili ya kuendana na Teknolojia ya ulimwengu wa sasa, nasi kama Wizara tumejipanga kutekeleza na kutimiza matarajio ya Rais kwa kuwezesha TBC kufanya Kazi kwa ufanisi zaidi” ameongeza Munaku

Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema TBC ina mipango ya kuwafikia wananchi zaidi kwa kuboresha usikivu wa Redio na vipindi vizuri vya televisheni ndani na nje ya Nchi

“TBC tumejitahidi Kuboresha vipindi vyetu na usikuvu Katika maeneo mengi lakini tunaendelea na juhudi ya Kuboresha zaidi usikivu katika maeneo ambayo bado tujafikia ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi” ameongeza Dkt Rioba

Mkutano huo wa baraza la wafanyakazi umefanyika kwa siku mbili na umehitimishwa leo jijini Dar es Salaam ambapo wajumbe wametoa maoni kuhusu mipango ya shirika ya shirika.