Tatueni changamoto za kiwanda cha chai Mponde

0
256

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu Deogratias Ndejembi amewataka watendaji wa Halmashauri ya Bumbuli wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga kuzitafutia ufumbuzi changamoto za miundombinu ya barabara na umeme katika kiwanda cha Chai cha Mponde.

Ndejembi ametoa rai hiyo wakati wa ziara yake katika kiwanda hicho ambacho Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umewekeza fedha kuhakikisha kinaendelea na uzalishaji na kuwa kimbilio la wakulima wa chai wilayani humo.

Akiwa kiwandani hapo Ndejembi amebaini kinakabiliwa na ukosefu wa umeme mara kwa mara na barabara mbovu ambazo zinaathiri uzalishaji na hivyo kuuelekeza uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Lushoto kushirikiana na uongozi wa kiwanda hicho kuhakikisha kunakuwa na umeme wa uhakika wakati wa uzalishaji.