Tasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoani Singida imefungua kesi mahakamani dhidi ya watumishi watatu wa halimashauri ya wilaya ya Singida wanaotuhumiwa kufanya ubadhirifu fedha zilizotengwa kwa ajili ya chanjo katika halimashauri.
Watumishi hao watatu wanatuhumiwa kwa kosa la matumizi mabaya ya mamlaka pamoja
na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 14 zilizotengwa kwa ajili ya
chanjo na hivyo kusababisha serikali kupata hasara.
Mkuu huyo wa TAKUKURU amezitaja taasisi zinazoongoza kwa rushwa kuwa ni
Halimashauri za wilaya ,Polisi na Mahakama ambapo pia katika kipindi cha
mizezi mitatu imeweza kuokoa zaidi ya shiling milioni 40 kupitia uchunguzi
uliofanywa na Takukuru kwenye taasisi mbalimbali za mkoa wa Singida.