TARURA yafungua barabara ya Unyianga-Mwankoko

0
195

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ummy Mwalimu ametembelea na kukagua ujenzi wa barabara mbadala ya Unyianga-Mwankoko kwa kipande cha Ziwa Kindai yenye urefu wa Kilomita 2.6 iliyopo Kata ya Unyianga katika Manispaa ya Singida.

Barabara hiyo inayojengwa kwa gharama ya shilingi Mililioni 263 ni barabara mbadala na mpya baada ya barabara ya awali kukatika Kutokana na mvua zilizonyesha mwaka 2019-2020.

Waziri Ummy amewapongeza viongozi wa mkoa huo hasa Mkuu wa Mkoa Dkt. Binilith Mahenge kwa kuwa na maono ya kufungua barabara mpya zitakazosaidia wanachi katika usafirishaji na pia kupendezesha mji wa Singida.

Aidha katika ukaguzi huo Waziri Ummy aliwashauri viongozi wa Mkoa wa Singida kusimamia upimaji na upangaji wa mji wa Singida na kuachana na makazi holela.

Barabara hiyo inahudumia wakazi wa Kata ya Unyianga- Mwankoko na Kata ya Mtamaa pia inaunganisha wakazi wa Wilaya ya Ikungi eneo la Minyughe na Manispaa ya Singida