Mbunge Janejelly Ntate ametaka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) uongezewe bajeti kwa kuwa una majukumu makubwa na unapaswa kupewa uhuru katika kuteleleza majukumu yake badala ya kuingiliwa na Wanasiasa kama ilivyo katika baadhi ya maeneo.
Ntate ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Amedai kuwa TARURA inaweza kupendekeza barabara fulani ijengwe lakini utashi wa kisiasa ukaingilia mipango hiyo na kuelekeza barabara nyingine ndio ijengwe jambo linaloleta mkanganyiko.