TANZIA: Salim Abdullah Turky afariki dunia

0
315

Mgombea ubunge wa Jimbo la Mpendae kupitia Chama cha Mapinduzi -CCM, Salim Abdullah Turky amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Marehemu Turky amefariki katika Hospitali ya Tasakhta Global Kisiwani Unguja.

Swala ya kuombea mwili wa marehemu inatarajiwa kufanyika leo alasiri katika msikiti wa Othman Maalim na kufuatiwa na mazishi yatakayofanyika Fumba visiwani humo.

Marehemu Salim Turky alikuwa mfanyabiashara maarufu Zanzibar na mgombea ubunge wa Jimbo la Mpendae kwa tiketi ya CCM.