TANZIA: Dkt. Shika Afariki dunia

0
446

Dkt. Louis Shika amefariki dunia katika Hospitali ya Nyanguge iliyopo Wilayani Magu, mkoani Mwanza.

Dkt. Shika alijizolea umaarufu nchini baada ya kutaka kununua nyumba za serikali kwa shilingi milioni 900.

Miongoni mwa misemo yake iliyojimtambulisha zaidi ni pamoja na “Tutaelewana tu kidogo kidogo, ngoja kwanza tuoneshane makali” na “Mia tisa itapendeza.”.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mwili wake utazikwa leo mkoani humo.