Tanzia: Balozi Kijazi afariki dunia

0
357

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametangaza kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, kifo cha Balozi Kijazi kimetokea majira ya saa 3:10 usiku katika Hospitali ya Benjamini Mkapa, jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa taratibu za mazishi ya marehemu Balozi Kijazi zitatangazwa hapo baadaye.