Tanzania na China kuongeza ushirikiano 2023

0
438

Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki amesema anatazamia kuona ushirikiano zaidi ukiendela kuongezeka baina ya China na Tanzania kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni ya sera mpya ya China ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya UVIKO 19 ambayo inapelekea kufunguliwa kwa milango ya kufanyika shughuli nyingi za kiuchumi baina ya mataifa hayo mawili.

Balozi Kairuki ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na vyombo vya habari vya China huku akieleza juu ya manufaa ya kuondolewa utaratibu wa ukaaji karantini kwa wasafiri wanaoingia China na kusema kuwa Tanzania itanufaika na safari za abiria na mizigo za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China kupitia kampuni ya ndege ya Air Tanzania ambapo pia itachochea ongezeko la watalii nchini kutokea China.

China hivi karibuni imeboresha hatua zake za kukabiliana na UVIKO 19 kwa kuondoa masharti ya kukaa karantini kwa wasafiri wanaoingia nchini humo.