Tanzania yavuna trilioni 2 kutoka Marekani

0
642

Tanzania inatarajiwa kuvuna uwekezaji wa takribani dola za Marekani bilioni 1 (sawa na zaidi ya shilingi trilioni 2.3) kutoka nchini Marekani.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache za kwanza za ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Marekani.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris wakati akizungumza na waandishi wa habari akiwa pomoja na mgeni wake, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Kamala amesema kuwa uwekezaji huo utawezesha ukuaji wa uchumi na kuzalisha ajira nchini Tanzania pamoja na Marekani, na kwamba nchi hizo zitaendelea kushirikiana katika masuala ya kiuchumi.

Mbali na hilo, viongozi hao wamezungumzia pia suala la afya hususani janga la UVIKO19.

Kwa upande wake Rais Samia amemwambia Makamu wa Rais Kamala kuwa uchaguzi wa kuizindulia programu ya Royal Tour nchini Marekani haukuwa wa bahati, bali walifanya hivyo wakijua kwamba nchi hiyo ndio sehemu kubwa zaidi ya starehe na burudani duniani.

Amesema anaamini jukwaa hilo litavutia watu wengi zaidi kuitembelea Tanzania na kujionea fursa za uwekezaji na utalii zilizopo kwenye nchi yenye maajabu.