Tanzania yatoshana nguvu na Sudan

0
182

Tanzania na Sudan zimetoshana nguvu katika mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA uliopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Sudan ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya kwanza ya mchezo, na Tanzania kusawazisha dakika ya 67.

Mara ya mwisho timu hizo kukutana ni mwaka 2019 ambapo Tanzania iliibuka kwa ushindi wa magoli 2-1.

Katika mchezo wa awali wa kirafiki Tanzania ilicheza dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1.