Tanzania yathibitisha askari wake kuuawa DRC

0
2062

Tanzania imethibitisha askari wake watatu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuuawa katika shambulio la bomu eneo la Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrsi ya Congo (DRC).

Katika taarifa yake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax amesema askari hao walikuwa wakifanya kazi chini ya misheni ya kulinda amani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Amesema askari wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea kwenye eneo la misheni hiyo.

Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ametoa pole kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi pamoja na ndugu, jamaa na marafiki kufuatia vifo vya askari hao.

Amesema askari hao watapumzishwa kwa heshima zote na taratibu za kijeshi.