Tanzania yasherehekea siku ya Uhuru

0
108

Watanzania leo wanaadhimisha miaka 61 ya Uhuru, Uhuru uliopatikana Desemba 9 mwaka 1961.

Maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Uhuru yamebeba kauli mbiu inayosema Miaka 61 ya Uhuru : Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo Yetu.

Katika kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru mwaka huu hakutakuwa na sherehe za Kitaifa, badala yake Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza shilingi milioni. 960 zilizotengwa kwa ajili ya sherehe hizo
zipelekwe Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule nane za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Maadhimisho hayo ya miaka 61 ya Uhuru yanafanyika kwa njia ya midahalo na makongamano yatakayofanyika katika wilaya zote nchini, yakitanguliwa na ratiba mbalimbali kwa viongozi wa mikoa na wilaya kufanya shughuli za kijamii.