Tanzania yapata msaada wa Bilioni 469

0
203

Serikali ya Tanzania na umoja wa ulaya zimesaini mikataba mitatu ya MSaada wenye thamani jumla ya Shilingi bilioni 469.4 kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa ushirikiano wa miaka saba baina ya umoja huo na TAnzania wa kuanzia mwaka 2021 – mpaka 2027.

Wakisaini makubaliano hayo jijini Dar es salaam, Katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Emanuel Tutuba amesema mikataba hiyo mitatu inalenga katika utekelezaji wa mradi wa kuboresha masuala ya jinsia,ambapo takribani Euro Milioni 70 ziatumika.

Katika fedha hizo pia kiasi cha Euro milion 75 zitaelekezwa kwenye ufadhili wa mradi ya kuifanya miji ya kuwa ya Kijani (Green and Smart cities, ) huku euro milioni 35 nazo zitaelekezwa katika ufadhili wa mradi wa Tanzania ya kidijitali (Digital for Tanzania ).

Aidha Tutuba ameuahakikisha ujumbe wa umoja wa Ulaya kuwa fedha hizo zitakwenda kutumika kama ilivyokusudiwa katika mikataba huo.