Tanzania yaongoza Afrika kwa usambazaji wa umeme

0
258

Waziri wa Nishati, Dkt Merdad Kalemani amesema Tanzania imekua nchi ya kwanza katika usambazaji wa umeme vijijini barani Afrika (73.4%) ikifuatiwa na Nigeria na Afrika Kusini.

Waziri Kalemani ameyasema hayo jijini Dodoma katika mkutano na wanahabari ambapo amebainisha kuwa jitihada hizo zimetokana na usimamizi wa miongozo ya serikali katika suala la usambazaji umeme vijijini.

Kwa upande mwingine Kalemani amesema serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili ya usambazaji umeme katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa majiji na manispaa ambapo tayari imeanza usambazaji huo katika Jiji la Dar es Salaam.