Tanzania yafanikiwa kudhibiti dawa za kulevya kwa asilimia 90

0
304

Kamishna wa Huduma za Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Valite Mwashusa amesema Tanzania imefanikiwa kudhibiti matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90.

Kamishna Mwashusa ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuhusu dawa za kulevya unaotarajiwa kufanyika nchini kuanzia Septemba 17 hadi 21 mwaka huu.

Amesema Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya dawa za kulevya, UNDC limeichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na imani yao katika juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. John Magufuli za kupambana na dawa za kulevya.