TANZANIA YAENDELEA KUUNGWA MKONO KIMATAIFA

0
173

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haijalipia kuweka tangazo la bendera ya Tanzania katika jengo refu kuliko yote duniani la Burj Khalifa lililopo Dubai, Falme za Kiarabu.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema tangazo hilo limewekwa kwa lengo la kuitangaza Tanzania kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

“Utawala wa Dubai umeweka tangazo hilo kwa kutambua ziara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan ameifanya Dubai na umeahidi kuendelea kuitangaza Tanzania kupitia jengo hilo maarufu katika kipindi cha ” amesema Dkt. Kijaji