Tanzania na Zambia kushirikiana katika maeneo saba

0
145

Tanzania na Zambia zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo saba ikiwemo kilimo, nishati, biashara na miundombinu.

Makubaliano hayo yamefikiwa baina ya Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, ambaye hii leo amefanya ziara ya siku moja hapa nchini.

Wakizungumza na waandishi wa habari Ikulu mkoani Dar es Salaam mara baada ya mazungumzo yao ya faragha, viongozi hao wamesema makubalian hayo yana lengo la kudumisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, viongozi hao wa Tanzania na Kenya pia wameshuhudia utiaji saini wa mikataba mitatu katika eneo la ulinzi na usalama, sanaa pamoja na utamaduni.