Tanzania na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba wa mashaurino ya Kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya ushirikiano wa kiuchumi.
Mikataba hiyo imesainiwa jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani nchini Mohammad Saleem.
Kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu kutasaidia kukuza na kuendeleza Diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.