Tanzania na India kushirikiana zaidi Kibiashara

0
150

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amewakaribisha wawekezaji wenye nia kutoka India kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali hususani viwanda vya kutengeneza dawa.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na India na Balozi wa India nchini Binaya Srikanta Pradhan.

Katika mazungumzo hayo, Dkt. Kijaji amemhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania iko tayari kupokea wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika sekta ya Anga, Utalii, Kilimo na Afya hususan katika viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kupunguza gharama za uagizaji dawa nje ya nchi.

Naye Balozi wa India nchini Tanzania Binaya Srikanta Pradhan amesema India imekuwa na uhusiano mzuri wa Kibiashara na uwekezaji na Tanzania hususani katika viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo, huduma za benki, madini na afya.