Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimesaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa posta, teknolojia na mawasiliano.
Utiaji saini huo umefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam ulishuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hasan na Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Rais Tshisekedi amesema kuwa sekta ya mawasiliano itakuza ushirikiano baina ya nchi hizi na kuzalisha maelfu ya ajira ambazo zitawanufaisha zaidi vijana wa nchi zote.