Tanzania na Canada kuendleza ushirikiano

0
217

Balozi wa Tanzania na Naibu Mwakilishi wa kudumu nchini Usiswi ,Hoyce Temu amekutana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Canada Patricia McCullagh na kuahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Kupitia Balozi huyo ,ameitakia Tanzania kheri katika uchaguzi ujao wa kiti cha Urais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani IPU na kufurahishwa na suala la kuwa na mwanamke katika kinyanganyiro hicho.

Tanzania ina uhusiano mzuri Canada wa muda mrefu kupitia SIDA na programu nyingine, Tanzania imekuwa ni moja ya nchi zilizonufaika na Uhusiano huo.