Tanzania na Burundi kuimarisha uhusiano

0
234

Rais Samia.Suluhu Hassan ambaye anaendelea na ziara yake nchini Burundi, pamoja na mwenyeji wake Rais Evarist Ndayishimiye wamekubaliana kuimarisha uhusiano kwa maslahi ya Wananchi wa pande zote mbili.
 
Amesema lengo la ziara yake ya siku mbili nchini Burundi ni kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya Tanzania na nchi hiyo.

Rais Samia Suluhu Hassan amewakaribisha Wafanyabiashara wa Burundi kuwekeza Tanzania, na kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yao.
 
Kwa upande wake Rais Evarist Ndayishimiye ameomba kuimarishwa kwa ushirikiano wa Tanzania na Burundi hasa katika ulinzi wa mpaka, na kwenye eneo kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya nchi kavu itakayotumika kuhifadhi mizigo ya Wafanyabiashara wa Burundi.