Tanzania na Bahamas kuanzisha ushirikiano rasmi

0
275

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba amekutana na Waziri wa Uhamiaji na Bima ya Taifa wa Bahamas, Alfred Sears pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaoendelea jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 15 hadi 20 Januari 2024.

Katika kikao hicho, viongozi hao wamesisitiza umuhimu wa nchi zao kuchukua hatua za haraka kuanzisha ushirikiano rasmi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.

Maeneo ya ushirikiano yatakayopewa kipaumbele ni pamoja na kukuza sekta ya utalii, biashara na uwekezaji, michezo na utamaduni.