Tanzania kukimbizana na kasi ya Dunia

0
285

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sodeyeka amesema Tanzania imejipanga kwenda na Kasi ya Mataifa mengine duniani katika ukuaji wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Prof. Sodeyeka amesema hayo Jijini Dodoma katika mkutano wa kuzungumzia Wiki ya Ubunifu na Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yatakayofanyika kitaifa Jijini Dodoma kuanzia tarehe 15 mwezi huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula amesema wiki ya ubunifu mwaka huu itaenda pamoja na kuwawezesha wabunifu nchini kuchangamkia fursa ya soko linalotokana na kazi za ubunifu wao duniani.

Wiki ya ubunifu mwaka huu, ambayo itaongozwa na kauli mbiu ya “ubunifu kwa maendeleo endelevu”, itafanyika pia Katika mikoa 16 nchini ambapo kutakuwa na shughuli mbali mbali zikilenga kuhamasisha ubunifu katika maeneo yao.