Tanzania kuhifadhi mafuta ya miezi 3

0
278

Tanzania inatarajia kuanza kuhifadhi akiba ya mafuta yatakayotumika katika kipindi cha zaidi ya miezi 3, tofauti na sasa ambapo inahifadhi kwa mujibu wa sheria kwa siku 15.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na waziri wa Nishati Januari Makamba, wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya serikali kupitia wizara ya Nishati na kampuni ya mafuta ya Erikali ya Falme za Kiarabu.

Waziri Makamba amesema serikali inataka kuwa na uhakika wa uhifadhi wa mafuta na kwamba ujio wa kampuni hiyo utasaidia kuboresha miundombinu ya bomba la kushusha mafuta bandarini na uhifadhi wa mafuta ya kutosha kwenye mikoa mbalimbali.