Tanzania kufungua rasmi ofisi za Ubalozi Indonesia

0
206

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stergomena Tax yupo Jakarta, Indonesia kwa ajili ya ziara ya kikazi ambapo atafungua rasmi ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini humo.

Akiwa nchini Indonesia Dkt. Tax pia anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Retno Marsudi na kutembelea chuo cha Diplomasia cha Indonesia.