Tanzania kuandaa mkutano wa SADC kwa mara ya mwisho

0
273

Waziri wa Mambo ya Nje, na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ametangaza kufanyika kwa mkutano wa mwisho wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), nchini Tanzania kabla ya uenyekiti kuchukuliwa na Msumbiji baadae mwaka huu.

Prof. Palamagamba Kabudi ameeleza kuwa Rais Magufuli aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa SADC mwaka 2019, akipokea kijiti kutoka kwa Rais wa Namibia, Dkt. Gottfried Geingob ambaye aliongoza jumuiya hiyo kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2019.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa kikao hicho cha SADC kitakachofanyika kati ya Machi 16 na 17, 2020.

Mkutano huo utahudhuriwa na mawaziri wa fedha na mipango; uchumi na biashara; pamoja na mawaziri wa mambo ya ndani kutoka nchi zote 16 za wanachama wa SADC.

Katika kipindi chake cha uenyekiti, Tanzania imeweza kuipaiza lugha ya Kiswahili katika nafasi za kimataifa.