Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesisitiza kuwa, hadi sasa Tanzania haina mshukiwa wala mgonjwa wa homa ya corona.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.
Hata hivyo Waziri Ummy Mwalimu amewaambia waandishi wa habari kuwa, pamoja na kwamba virusi hivyo havijaingia nchini bado tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa ya kujikinga.
Amesema tayari serikali imeandaa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na virusi hivyo ikiwa ni pamoja na kuwatayarisha wataalamu wa afya katika maeneo ambayo yana uwezekano wa kufikiwa na wageni kutoka nje ili waweze kuwafanyia uchunguzi wa awali.
Virusi hivyo vya corona vilivyoanzia katika mji wa Wuhan nchini China, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu mbili katika nchi mbalimbali huku wengine zaidi ya elfu 83 wakiugua homa hiyo ya corona.