Tanga yapokea msaada wa mitungi 50 ya oxygen

0
253

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amepokea msaada wa mitungi 50 ya oxygen kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji msaada wa kupumua.

Mara baada ya kupokea msaada huo uliotolewa na Kampuni ya Oxygen Product East Africa iliyopo jijini Tanga, Shigella ameuagiza uongozi wa Hospitali ya Mkoa ya Bombo kutawanya mitungi hiyo katika vituo vya afya 22 vilivyopo mkoani humo.

Aidha, amesema msaada huo umekuja kwa wakati, na kwamba mitungi hiyo inaweza kusaidia wagonjwa 100 kwa wakati moja.

Mkoa wa Tanga umepokea zaidi ya shilingi bilion 21 kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya.