TANESCO Yatakiwa Kupeleka Umeme Vijijini Mkoani Iringa

0
190

Waziri wa Nishati Dokta Medard Kalemani ameliagiza Shirika la umeme nchini TANESCO pamoja na watendaji wa REA kupeleka umeme katika vijiji vya kata ya Ikweha na Sadani mkoani Iringa ili kuwapatia wananchi huduma hiyo waliyoisubiri kwa muda mrefu.

Waziri wa Nishati Dokta Medard Kalemani

Akizungumza na wananchi wa kata hizo, Waziri Kalemani pia ameiagiza TANESCO kufungua ofisi ndogo za malipo kila Kijiji kwa lengo la kuwapunguzia wananchi gharama za kuunganisha umeme.

Waziri Kalemani amezungumza na  Wananchi wa vijiji vya kata za Ikweha na Sadani wakati alipofika kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na kuwapa matumaini kuunganishwa umeme siku za karibuni.